Follow by Email

Thursday, January 18, 2018

Tanzania yashiriki maonesho ya utalii ya kimataifa nchini Uholanzi


Washiriki kutoka Tanzania wakiwa katika banda la Tanzania kwenye Maonesho maarufu ya Utalii ya Kimataifa (Vakantiebeurs 2018) yaliyofanyika hivi karibuni mjini Utrecht, Uholanzi.

Kutoka kushoto ni Bw. Willy Lyimo wa Bodi ya Utalii (TTB), Bibi Agnes Kiama Tengia, Afisa Ubalozi, Bw. Susuma Kusekwa wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), Bw. John Sung’are wa African Wildcats Expeditions Ltd. (Arusha), Bibi Naomi Z. Mpemba, Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Tanzania The Hague Uholanzi na Bw. Mushtaqali Abdalla wa Bobby Tours and Safaris (Arusha).

Kaimu Balozi Bibi Naomi Z. Mpemba akimsikiliza mteja aliyefika kwenye banda la Tanzania.

Bw. Iddi Mavura wa NCAA na Bw. Susuma Kusekwa wa TANAPA wakiwasiliza wateja waliofika kwenye banda la Tanzania katika Maonesho ya Utalii ya Kimataifa ya Vakantiebeurs 2018.

Bi. Sophia Tumsifu, Mtumishi wa Ubalozi akiwapa maelezo wateja waliofika katika banda la Tanzania ambapo pamoja na kupata taarifa kuhusu vivutio vya Tanzania, walipata pia ladha ya vyakula vya Tanzania.

Bibi Mwajuma Kitano, Mwanamuziki Mtanzania anayeishi Uholanzi, akiwa pamoja na wanafunzi wake ambao ni raia wa Uholanzi, kwa pamoja wakitumbuiza katika banda la Tanzania katika Maonesho ya Utalii ya Kimataifa ya Vakantiebeurs 2018.